Kampuni ya China yatoa vitabu zaidi ya 500 kwa chuo kikuu cha Misri
2023-11-29 09:05:14| CRI

Kampuni ya mafuta ya petroli ya China Sinopec imetoa zaidi ya vitabu 500 kwa Chuo Kikuu cha China cha Misri (ECU), vyenye mchanganyiko wa lugha za Kichina, Kiarabu, Kichina-Kiarabu, na Kichina-Kiingereza, vikihusu mambo ya dawa za jadi za Kichina, utamaduni wa Kichina, fedha, uchumi, usimamizi, biashara ya mtandaoni na ufundishaji wa lugha ya Kichina.

Akiongea mjini Cairo kwenye hafla ya kukabidhi vitabu hivyo, ofisa mwandamizi wa ubalozi wa China nchini Misri Lu Chunsheng, amesema huu ni mwaka wa kumbukumbu ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwa pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia moja”(BRl), na China na Misri ni washirika wa asili katika ujenzi wa ukanda huo.

Bwana Lu amesema vitabu hivyo vitawapa walimu na wanafunzi mtazamo mpya wa kuthamini utajiri wa historia, utamaduni na lugha ya China, na kupata ufahamu kuhusu maendeleo ya jamii ya kisasa ya China.