Kenya yakumbatia mageuzi kuwashirikisha wakimbizi kwenye jamii
2023-11-29 08:20:32| CRI

Kenya imeanza kutelekeza mageuzi yatakayowashirikisha wakimbizi kwenye jamii ili kuongeza kiwango chao cha kujitegemea na ustahimilivu.

Katibu mkuu wa Wizara ya Uhamishaji na Huduma za Raia, Julius Bitok ameliambia jukwaa moja la kimataifa mjini Nairobi kuwa kambi za wakimbizi zinabadilishwa kuwa makazi shirikishi ili kuhakikisha ushirikishwaji wa kiuchumi na kijamii kwa wakimbizi na jamii zinazowapokea.

Kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Wakimbizi, Kenya imepokea wakimbizi na watafuta hifadhi zaidi ya 630,000.

Bw. Bitok amesema mageuzi yanayoendelea sasa pia yanahusisha kuongeza upatikanaji wa uandikishaji na huduma za umma kwa wakimbizi kabla ya mwaka 2027.