Semina ya China na Ethiopia yahimiza ushirikiano wa kuimarishwa katika maendeleo ya elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi
2023-11-30 08:47:15| CRI

Wataalamu na watunga sera waliohudhuria semina ya ngazi ya juu kuhusu ushirikiano kati ya China na Afrika katika elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi (TVET) na vigezo vya kazi, wametoa wito wa kuimarishwa kwa ushirikiano kati ya China na Ethiopia katika maendeleo ya elimu hiyo.

Semina hiyo ya Mabadilishano ya Kiakademia ya China na Ethiopia kuhusu Marekebisho na Maendeleo ya Viwango vya Kazi na Maonesho ya TVET, ilifanyika jumatano Addis Ababa, ikiwashirikisha maofisa wakuu wa serikali ya Ethiopia, wenzao wa China, wasomi na wataalam mbalimbali.

Wataalam na wawakilishi kutoka nchi zote mbili walijadili na kubadilishana uzoefu kuhusu marekebisho na maendeleo ya vigezo vya kazi, pamoja na ukuzaji na matumizi yao ndani ya sekta ya elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi.

Taasisi na vyuo 11 kutoka Mkoa wa Shaanxi wa China, vinavyobobea katika nyanja mbalimbali kama vile uzalishaji kwa kutumia akili bandia, usafiri wa anga, nishati, fedha, vifaa, hifadhi ya maji, kilimo na uhandisi wa reli, zilichangia utaalamu wao na wenzao wa Ethiopia.