Mkutano wa 28 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Kimataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP28) umefunguliwa leo huko Dubai.
Kulingana na utafiti uliofanywa na Shirika la Kimataifa la Televisheni la China (CGTN), kati ya watumiaji wa mtandao duniani, asilimia 90.3 ya waliohojiwa wanaamini kuwa hakuna nchi inayoweza kuepuka changamoto ya mabadiliko ya tabianchi, na utaratibu wa pande nyingi ni njia ya msingi ya kutatua changamoto hiyo, na asilimia 91.4 ya waliohojiwa wamepongeza China kwa mchango wake katika kuhimiza juhudi za kushughulikia changamoto hiyo duniani.
China imekuwa ikishiriki kikamilifu katika juhudi za kimataifa za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Karibu nusu ya uwezo wa uzalishaji wa umeme kwa nishati ya jua duniani uko nchini China, zaidi ya nusu ya magari ya nishati mpya duniani yanatumiwa nchini China, na robo ya eneo jipya la kijani duniani linatoka China.