Rais wa China atoa salamu za rambirambi kwa rais wa Marekani kufuatia kufariki kwa Bw. Henry Kissinger
2023-11-30 21:14:13| CRI

Rais wa China Xi Jinping leo Alhamisi ametoa salamu za rambirambi kwa rais wa Marekani Joe Biden kufuatia kufariki kwa aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw. Henry Kissinger.

Katika salamu hizo, rais Xi amesema China iko tayari kushirikiana na Marekani kuimarisha urafiki kati ya watu wa nchi hizo mbili, kuhimiza maendeleo mazuri ya uhusiano kati ya pande hizo mbili, ili kuwanufaisha wananchi wao, na kutoa mchango kadiri iwezavyo kwa amani na maendeleo ya dunia.