Shirika la ndege la Kenya kurejesha safari za ndege za wiki kwenda Somalia
2023-11-30 08:55:16| CRI

Shirika la ndege la Kenya KQ limesema litarejesha safari za ndege za moja kwa moja kwenda Mogadishu kutoka Nairobi kuanzia Februari mwaka kesho, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuhimiza biashara na kurahisisha usafiri wa watu wanaovuka mpaka.

Ofisa mkuu wa kibiashara na wateja wa Shirika hilo Bw. Julius Thairu amesema kurejeshwa kwa safari za ndege kunatokana na kuongezeka kwa biashara na idadi ya safari za ndege kati ya nchi hizo mbili.

Bw. Thairu ametoa taarifa ikisema wana matarajio makubwa kuhusu uwezekano wa kujenga tena uhusiano kati ya Kenya na Somalia kupitia Shirika la KQ. Pia amesema shirika hilo linafanya juhudi kutoa huduma bora kwa wateja, kuhimiza kwa pamoja biashara na uwekezaji ili kutimiza ukuaji wa kudumu.

Urejeshwaji huo unafuatia kusimama kwa muda tangu Agosti 2020 kwa lengo la kuzuia kuenea kwa maambukizi ya COVID-19.