China iko tayari kuimarisha uhusiano na ushirikiano na Kazakhstan
2023-11-30 14:46:00| cri

Naibu Waziri Mkuu wa China Ding Xuexiang amesema China iko tayari kushirikiana na Kazakhstan ili kutekeleza makubaliano muhimu yaliyofikiwa na wakuu wa nchi hizo mbili, kukuza ujenzi wa hali ya juu wa pendekezo la Ukanda Mmoja Njia Moja (BRI), na kuendeleza ushirikiano wa kudumu wa kimkakati kati ya China na Kazakhstan na kufikia ngazi ya juu zaidi.

Ding, ambaye alifanya ziara nchini Kazakhstan kuanzia Novemba 26 hadi 27, aliyasema hayo alipokutana na Rais wa Kazakh Kassym-Jomart Tokayev mjini Astana.

Akibainisha kuwa ushirikiano kati ya China na Kazakhstan una msingi imara, uwezo mkubwa na matarajio mapana, Ding amesisitiza kuwa China iko tayari kushirikiana na Kazakhstan ili kuimarisha msingi wa kuaminiana, kuimarisha ushirikiano wa mikakati ya maendeleo, kuimarisha uratibu wa sera na kupanua ushirikiano wa kunufaishana ili kusaidiana kufikia malengo yao ya maendeleo.

Kwa upande wake Tokayev alisema Kazakhstan inapenda kushirikiana na China ili kuzidisha ushirikiano wa kivitendo katika nyanja mbalimbali, kukabiliana kwa uthabiti na "nguvu tatu" za ugaidi, kuimarisha mawasiliano kati ya watu na ushirikiano wa mataifa madogo, na kuleta mafanikio mapya katika ushirikiano wa kimkakati wa kina na wa kudumu kati ya nchi hizo mbili.