WFP na UDSM wasaini mkataba wa tathmini ya usalama wa chakula nchini Tanzania
2023-11-30 14:04:42| cri

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limeingia mkataba wa muda mrefu na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ili kuimarisha tathmini ya usalama wa chakula na lishe nchini.

Mkataba uliotiwa saini Jumatano una thamani ya Sh542 milioni na utekelezaji wake unatazamiwa kuwa kwenye programu za WFP, na kuleta ujuzi wa kitaalamu katika maendeleo ya jamii.

Chini ya awamu ya pili ya Mpango Mkakati wa Nchi wa miaka mitano (CSP) uliozinduliwa Julai 2022, WFP Tanzania inaongoza mipango kadhaa inayolenga kuimarisha usalama wa chakula na lishe.

Kwa mujibu wa WFP, ushirikiano na UDSM unaelenga kuwa na matokeo ya ziada na kutoa nafasi zaidi ya kuboreshwa katika utekelezaji wa programu kupitia tathmini za mara kwa mara.