Katibu mkuu wa Chama cha CCM Tanzania ajiuzulu
2023-11-30 08:36:15| CRI

Katibu mkuu wa chama tawala cha Tanzania CCM, Daniel Chongolo amejiuzulu.

Kujiuzulu kwake kulitangazwa na Paul Makonda, katibu wa itikadi na uenezi wa CCM mwishoni mwa mkutano wa siku mbili wa Halmashauri kuu ya CCM (NEC) uliofanyika mjini Dar es Salaam. Bw. Makonda hakueleza sababu ya kujiuzulu kwa Bw. Chongolo, ambaye aliteuliwa kuwa katibu mkuu wa CCM mwezi Aprili mwaka 2021.