Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano wa pili wa AfCFTA kuhusu Wanawake katika Biashara
2023-11-30 14:06:45| cri

Serikali ya Tanzania imekamilisha maandalizi ya Rasimu ya Itifaki ya Wanawake na Vijana katika Biashara ndani ya Makubaliano ya Eneo la Biashara Huria la Afrika (AfCFTA).

Itifaki hiyo sasa inasubiri kuidhinishwa na mawaziri wa biashara wa AfCTA ili kuanza kutumika mwaka 2023/24.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Ashatu Kijaji ameyasema hayo jana Novemba 29, 2023 alipokuwa akitoa taarifa kwa vyombo vya habari, ambapo ameeleza kuhusu mkutano huo wenye kaulimbiu ya “Kuimarisha Ushiriki wa Wanawake katika Biashara na Kuharakisha Utekelezaji wa AfCFTA” ulioandaliwa na wizara kwa kushirikiana na Sekretarieti ya AfCFTA, ambapo Tanzania itakuwa mwenyeji.