Mafuriko yasababisha vifo 270 na makumi ya maelfu ya watu kukimbia makazi katika Pembe ya Afrika
2023-11-30 08:34:33| CRI

Kituo cha Utabiri na Matumizi ya Hali Hewa (ICPAC) cha Mamlaka ya Kiserikali ya Maendeleo ya Nchi za Afrika Mashariki (IGAD) kimesema, karibu watu 270 wamefariki dunia na zaidi ya 900,000 wamelazimika kukimbia makazi yao kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua inayoendelea kunyesha katika Pembe ya Afrika.

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na kituo hicho, Kenya, Ethiopia na Somalia zimeathirika vibaya zaidi na mvua za El Nino pamoja na hali ya hewa ya IOD (Indian Ocean Dipole), na idadi ya jumla ya walioathiriwa na mafurikio inakadiriwa kuwa ni watu milioni 1.5 nchini Somalia, 950,000 nchini Kenya na 101,890 nchini Ethiopia.