Umoja wa Afrika watoa wito kwa nchi za Afrika kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na wasichana
2023-11-30 09:07:36| CRI

Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat ametoa wito kwa nchi za Afrika kuchukua hatua madhubuti kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na wasichana.

Bw. Faki alitoa wito huo kwenye taarifa iliyotolewa Jumanne wiki hii ambapo Harakati ya Siku 16 za Kutokomeza ukatili dhidi ya Wanawake na Wasichana ikiendelea. Amesisitiza kuwa hatua madhubuti na zenye ufanisi zinahitajika kwa ajili ya kujenga jamii iliyoshirikishi, salama na yenye usawa, ambayo inaweza kulinda haki za wanawake na wasichana. Pia ametoa wito kwa nchi za Afrika kutenga bajeti maalumu kwa ajili ya kuzuia ukatili dhidi ya wanawake na wasichana, na kuwasaidia wahanga wa ukatili wa kijinsia.