Wizara ya Mambo ya Nje ya China yatoa waraka wa msimamo wa China juu ya utatuzi wa mgogoro kati ya Palestina na Israel
2023-11-30 14:07:48| cri

Wizara ya Mambo ya Nje ya China leo tarehe 30 Novemba imetoa waraka wa msimamo wa China juu ya utatuzi wa mgogoro kati ya Palestina na Israel.

Waraka huo ulisema mgogoro huo umesababisha vifo na majeruhi ya raia wengi, pamoja na janga la kibinadamu, ambapo jumuiya ya kimataifa inafuatilia zaidi mgogoro huo.

Kwa mujibu wa Katiba ya Umoja wa Mataifa, China inatoa mapendekezo yafuatayo: Kwanza, kusitisha vita kwa pande zote. Pili, kuwalinda raia ipasavyo. Tatu, kuhakikisha msaada wa kibinadamu. Nne, kuimarisha usuluhishi wa kidiplomasia. Tano, kutafuta utatuzi wa kisiasa.