Rais Xi Jinping wa China ameahidi kwamba China itaendelea na juhudi za kutetea haki katika suala la Palestina, kuhimiza mazungumzo ya amani na kama kawaida kutoa misaada ya kibinadamu na maendeleo kwa watu wa Palestina.
Katika salamu za pongezi kwa mkutano wa Umoja wa Mataifa uliofanyika Jumatano kwa ajili ya kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Mshikamano na Watu wa Palestina, Xi alisema China, ikiwa ni mwanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, itaendelea kushirikiana na jumuiya ya kimataifa ili kujenga maelewano ya kimataifa kwa ajili ya kuhimiza amani, na kurudisha suala la Palestina kwenye njia sahihi ya mpango wa nchi mbili kwa ajili ya suluhu ya kina, ya haki na ya kudumu mapema.