Aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wa Marekani Henry Kissinger afariki dunia akiwa na umri wa miaka 100
2023-11-30 14:48:22| cri

Aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wa Marekani Henry Kissinger amefariki dunia jana Jumatano nyumbani kwake Connecticut akiwa na umri wa miaka 100a.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kissinger Associates, akiwa Waziri wa Mambo ya Nje chini ya marais Nixon na Ford, Dkt. Kissinger "alibeba jukumu kubwa katika kufungua milango kwa China, kujadili mwisho wa Vita vya Yom Kippur katika Mashariki ya Kati, na kusaidia kumaliza jukumu la Marekani katika Vita vya Vietnam.

Taarifa hiyo imeendelea kusema kuwa Dkt. Kissinger ameandika vitabu 21 kuhusu masuala ya usalama wa taifa. Akichukuliwa kama mmoja wa viongozi mashuhuri wa Marekani, Dkt. Kissinger alitakiwa ushauri mara kwa mara na marais wa Marekani wa vyama vyote vya siasa na viongozi wengi wa kigeni baada ya kumaliza utumishi wake serikalini mwaka 1977.