Wadhibiti wa elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi barani Afrika (TVET) Alhamisi walianza mkutano mjini Nairobi, ili kuandaa mpango wa kuoanisha vigezo vya maeneo hayo.
Mkutano huo wa siku mbili unaohudhuriwa na viongozi wa mashirika ya udhibiti wa elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi kutoka barani kote, pia una lengo la kuimarisha mabadiliko ya kidijitali na usimamizi wa mifumo ya elimu na mafunzo ya ufundi stadi.
Mshauri mkuu wa vijana katika Idara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ubunifu ya kamisheni ya Umoja wa Afrika (AUC) Bw. Nicholas Ouma, amesema tume hiyo ina nia ya kufufua mafunzo ya ufundi katika bara la Afrika. Amesema lengo ni kusaidia kuwawezesha vijana kuleta mageuzi ya haraka katika viwanda ili kuchangia maendeleo.