WHO yataka uingiliaji unaoongozwa na jamii ili kutokomeza ugonjwa wa UKIMWI barani Afrika
2023-12-01 09:20:18| CRI

Ofisa wa Shirika la Afya Duniani (WHO) amesema kabla ya Siku ya Kupambana na UKIMWI Duniani kwamba kufikia lengo la kutokomeza ugonjwa wa UKIMWI barani Afrika ifikapo mwaka 2030, kutategemea msaada zaidi wa hatua zinazoongozwa na jamii za kinga na matibabu.

Mkurugenzi wa shirika hilo barani Afrika Bw. Matshidiso Moeti, amesema kaulimbiu ya Siku ya Kupambana na UKIMWI Duniani mwaka huu ni "Jamii Ziongoze," ikisisitiza haja ya kujitolea na uvumbuzi ili kufikia malengo ya kutokomeza UKIMWI barani Afrika ifikapo 2030.

Amesema uongozi thabiti wa jamii ni muhimu katika kupunguza maambukizi ya UKIMWI na vifo barani Afrika kupitia kampeni za uhamasishaji, upatikanaji wa matibabu, na kupiga vita unyanyapaa.