UM: Mafuriko nchini Ethiopia yawaathiri watu milioni 1.5 na kuwalazimisha watu laki 6 kukimbia makazi
2023-12-01 08:47:26| CRI

Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoratibu masuala ya kibinadamu OCHA imesema, mafurikio yaliyotokea mwezi uliopita nchini Ethiopia yamewaathiri watu milioni 1.5, na kuwalazimisha watu laki sita kukimbia makazi yao.

Kwa mujibu wa OCHA, asilimia 80 ya waathirika wa mafuriko wako katika jimbo la Somali, ambako maafa hayo yamesababisha hasara kubwa kwa mazao, mifugo na miundombinu muhimu, na kuleta hatari kubwa ya kutokea milipuko ya magonjwa ya kuambukiza kama vile kipindupindu, malaria na homa ya dengue.

OCHA imesema mpango wa msaada wa kibinadamu nchini Ethiopia kwa mwaka huu unahitaji dola za kimarekani bilioni 4, lakini mpaka sasa ni theluthi moja ndio zimepatikana.