Umoja wa Afrika wasisitiza tena mshikamano wa Afrika na watu wa Palestina
2023-12-01 09:12:18| CRI

Mwenyekiti wa  Tume ya Umoja wa Afrika Bw. Moussa Faki Mahamat amesisitiza tena mshikamano wa Afrika na watu wa Palestina. 

Mwenyekiti huyo amesema hayo katika taarifa iliyotolewa jumatano katika shughuli ya kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Mshikamano na Watu wa Palestina.

Bw. Faki amesema siku hiyo ya kimataifa ya mshikamano na watu wa Palestina inayoadhimishwa kila mwaka, ni siku ya kusisitiza tena jumuiya ya kimataifa kuendelea kufanya juhudi kuunga mkono shughuli ya haki ya uhuru na taifa kwa Palestina. 

Bw. Faki amesema, shughuli ya watu wa Palestina ni ya dharura sana. Matukio ya uhasama yanayoendelea katika ukanda wa Gaza na kukaliwa kwa ardhi, ni ukiukwaji dhahiri wa sheria ya kimataifa na sheria ya kibinadamu ya kimataifa, ambao umeleta athari kwa maisha ya raia wa Palestina na kwa amani katika kanda hiyo kwa ujumla.