NBA yazindua ofisi nchini Kenya
2023-12-01 13:50:47| cri

Ni mwanga mpya kwa mpira wa kikapu nchini Kenya kufuatia kuzinduliwa kwa ofisi ya Shirikisho la Kitaifa la Mpira wa Kikapu (NBA) jijini Nairobi.

Bingwa mara tano wa NBA Ron Harper, Afisa Mkuu Mtendaji wa NBA Afrika Victor Williams na Rais wa Ligi ya Kikapu Afrika (Bal) Amadou Gallo Fall ni miongoni mwa watu mashuhuri waliohudhuria hafla hiyo iliyofanyika Jumatano jioni katika Hoteli ya Sankara jijini Nairobi.

Wengine ni pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa NBA Kenya na Kiongozi wa Uendeshaji Nchini Michale Finley, Mkuu wa Operesheni za Mpira wa Kikapu wa NBA Afrika Frank Traore na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu la Kenya Paul Otula.

Mapema siku hiyo, Harper alimtembelea Rais William Ruto katika ikulu ya Nairobi kabla ya kuandaa kliniki ya mpira wa kikapu kwa wachezaji 70 chipukizi wa mpira wa kikapu katika Shule ya Kimataifa ya Sabis, Runda jijini Nairobi.

Ruto alitaja mpango huo kuwa hatua ya mabadiliko katika maendeleo ya mchezo huo nchini. Alisema hatua hiyo itawapa vijana wa Kenya fursa ya kujiendeleza kitaaluma kwenye mchezo huo.