Kituo cha biashara kilichojengwa kampuni ya China nchini Tanzania chahimiza ajira na kukuza uchumi
2023-12-01 08:46:49| CRI

Kituo cha biashara na ugavi kilichojengwa na kampuni ya China nchini Tanzania kilichopangwa kufunguliwa kwa majaribio mwezi Julai mwaka 2024 nchini Tanzania, kimetoa maelfu ya nafasi za ajira kwa wenyeji na kinatarajiwa kuchochea ukuaji wa uchumi wa nchi hiyo.

Mradi wa Kituo cha Biashara na Ugavi cha Afrika Mashariki chenye eneo la mita za mraba 75,000 kwa ajili ya maduka elfu mbili pamoja na maegesho, unafadhiliwa na Kampuni ya Kituo cha Biashara na Ugavi cha Afrika Mashariki EACLC, ambayo ni kampuni ya China inayojishughulisha na biashara ya kimataifa, na ujenzi wake unatekelezwa na Kampuni ya uhandisi wa kiraia ya CCECC ya China.