TRA yatambua Huawei Tanzania kama Mlipakodi Mzuri Zaidi
2023-12-02 22:51:12| cri

Katika hafla iliyohudhuriwa na Naibu Waziri Mkuu, Dk Dotto Biteko, Huawei Tanzania ilitunukiwa tuzo na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa uwajibikaji wake wa kupigiwa mfano wa kulipa kodi. Kampuni hiyo kubwa ya teknolojia iliibuka kama mlipa kodi anayetii sheria zaidi katika sekta ya teknolojia na mlipa kodi mtiifu zaidi kisekta na ngazi ya kitaifa.

Akikabidhi Tuzo ya Kila Mwaka ya Kuthamini Mlipakodi 2023, Dk. Diteko, ambaye pia ni Waziri wa Nishati alisema walipakodi wanapaswa kuchukuliwa kama washirika katika maendeleo ya nchi.

Mchango wa kampuni hiyo nchini Tanzania umekuwa mkubwa na kuvuka michango yake ya kijamii, hasa katika kutekeleza jukumu muhimu la kuendeleza miundombinu ya teknolojia na muunganisho wa kidijitali. Huawei imekuwepo nchini Tanzania kwa miaka 17 tangu 2007 na imekuwa mchangiaji mkubwa zaidi wa miundombinu ya TEHAMA nchini, ikihudumia asilimia 75 ya watu wote.

Kwa sasa, Huawei imeanzisha ushirikiano na vyuo vikuu 19 vya ndani na imejenga maabara 4 za mazoezi ya TEHAMA. Zaidi ya walimu na wanafunzi 3,000 wamepatiwa mafunzo na Akademi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ya Huawei.