Rais Xi Jinping wa China atoa barua ya pongezi kwa Jukwaa la kwanza la Liangzhu
2023-12-03 12:07:08| CRI

Rais Xi Jinping wa China ametoa barua ya pongezi leo tarehe 3 kwa Jukwaa la kwanza la Liangzhu.

Rais Xi ameeleza kuwa Magofu ya Akiolojia ya Liangzhu ni thibitisho halisi la historia ya ustaarabu wa taifa la China wa miaka elfu tano na pia ni hazina adimu kati ya staarabu za dunia. Ustaarabu wa taifa la China limeweka vilele mbalimbali vya kiustaarabu kwa uvumbuzi na ustahimilivu wake uliorithiwa kizazi baada ya kizazi, na pia umerutubisha staarabu za dunia ambapo umekuwa ukishikilia kujiendeleza na kujumuisha sifa bora za staarabu anuwai duniani.
Rais Xi amesisitiza kuwa kuheshimiana, kushikamana na kuishi kwa masikilizano ni njia sahihi kwa kuendeleza staarabu za binadamu. Anatumai pande mbalimbali husika ziweze kutumia jukwaa hili kuimarisha mawasiliano kati ya staarbu na nchi zinazoshiriki kwenye ujenzi wa pamoja wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, kutekeleza Pendekezo la Ustaarabu Duniani na kuhimiza watu wa nchi mbalimbali kuelewana na kusikilizana.

Jukwaa la awamu ya kwanza la Liangzhu lenye kaulimbiu ya “Kutekeleza Pendekezo la Ustaarbu Duniani, kuhimiza mawasiliano na mabadilishano kati ya staarabu” limefunguliwa leo mjini Hangzhou, mkoani Zhejiang, China.