Argentina yatunuku nishani ya “mafanikio makubwa katika ushirikiano na mawasiliano ya kiutamaduni ya kimataifa” kwa mkuu wa CMG
2023-12-03 13:59:22| CRI

Serikali ya Argentina Desemba mosi ilitunuku nishani ya “mafanikio makubwa katika ushirikiano na mawasiliano ya kiutamaduni ya kimataifa” kwa mkuu wa Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG) Bw. Shen Haixiong wakati ubalozi wa Argentina nchini China ulipofanya shughuli za mabadilishano kuhusu mazao ya ushirikiano kati ya watu wa nchi hizo mbili. Bw. Shen ametunukiwa nishani hiyo na balozi wa Argentina Sabino Vaca Narvaja kwa niaba ya rais Alberto Fernandez kwa mchango wake katika kuimarisha mawasiliano ya kiutamaduni kati ya China na Argentina na kuhimiza urafiki kati ya watu wao.

Rais wa Argentina Alberto Fernandez ametoa hotuba kwa njia ya video akisema kuwa chini ya uongozi wa rais Xi Jinping, watu wa China wametoa msaada kwa Argentina wakati nchi hiyo ilipokumbwa na taabu, na Argentina itaendelea kushirikiana na China kukabiliana na changamoto katika zama za leo. Bw. Shen alisema kwenye hotuba yake kwamba CMG linatekeleza mapendekezo matatu yaliyotolewa na rais Xi likijenga mfumo wa ushirikiano wa muda mrefu na vyombo vikuu vya habari vya Argentina na litaendelea kutoa mchango katika kuhimiza maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili.