Bukina Faso na Niger zaamua kujiondoa kwenye kundi la Sahel
2023-12-04 10:15:50| CRI

Ofisi ya habari ya serikali ya mpito ya Bukina Faso tarehe 2 imetangaza kwamba nchi hiyo na Niger zimeamua kujiondoa kwenye mashirika yote ya kundi la nchi tano la Sahel.

Habari zinasema, kwa mujibu wa taarifa ya pamoja ya Bukina Faso na Niger iliyosainiwa tarehe mosi, baada ya kuchunguza kwa kina kundi la Sahel na uendeshaji wake, nchi hizo mbili zimeamua kujiondoa kwenye mashirika yote ya kundi la Sahel, ikiwa ni pamoja na kikosi cha pamoja cha kupambana na ugaidi.

Taarifa inasema, madhumuni ya kuanzisha kundi la Sahel ni kuhimiza usalama na maendeleo ya kanda ya Sahel, lakini miaka 9 iliyopita inaonekana ni ngumu kutimiza. Bukina Faso na Niger zinashikilia kujitahidi kutimiza amani ya kudumu ya Sahel, na zinapenda kubeba majukumu yote ya kujiondoa kwenye kundi hilo.