Sudan yasema mazungumzo ya amani yatakayoshindwa kutimiza matakwa ya watu wa nchi hiyo hayatakubalika
2023-12-04 11:05:04| cri

Mwenyekiti wa Baraza la Mpito la Utawala wa Sudan na Kamanda wa Jeshi la nchi hiyo, Jenerali Abdel Fattah al-Burhan amesema, mazungumzo yoyote ya amani ambayo yatashindwa kutimiza matakwa ya Wasudan hayatakubalika.

Taarifa iliyotolewa na Baraza hilo imesema, Jenerali Al-Burhan ameahidi kuwa jeshi la nchi hiyo litaendelea na kupambana na Kikosi cha Mwitikio wa Haraka (RSF). Pia amesisitiza kuwa, Sudan iko tayari kushirikiana na jamii ya kimataifa, na kumkaribisha mjumbe mpya wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan, Ramtane Lamamra, huku akionya kuwa, nchi hiyo haiko tayari kupokea mjumbe anayependelea upande ama kundi lolote.