Serikali ya Kenya kupendekeza sheria ya kudhibiti soko la hewa ukaa nchini humo
2023-12-04 11:06:08| cri

Rais wa Kenya William Ruto amesema serikali yake inapanga kuwasilisha bungeni sheria itakayothibiti soko la hewa ukaa nchini humo kwa lengo la kukabiliana na udanganyifu katika biashara hiyo.

Akiongea katika kongamano la Umoja wa Mataifa la Mabadiliko ya Tabianchi (COP28) lililofanyika Dubai, Falme za Kiarabu (UAE), Rais Ruto amesema tayari mipango inaandaliwa kuwasilisha muswada bungeni ambao kama ukiridhiwa, utakuwa sheria ya kudhibiti biashara hiyo ya hewa ukaa.

Rais Ruto pia amesema Kenya inaunga mkono mpango wa Benki ya Dunia kudhibiti soko la hewa ukaa duniani ili kuhakikisha usawa, haki na uwazi katika biashara hiyo.