Idadi ya vifo vinavyotokana na mafuriko na maporomoko ya udongo nchini Tanzania yafikia 47
2023-12-04 10:24:53| CRI

Idadi ya watu waliofariki kutokana na mafuriko na maporomoko ya udongo yaliyosababishwa na mvua kubwa kaskazini mwa Tanzania imepanda kutoka 23 iliyotangazwa awali hadi 47 Jumapili jioni.

Akiongea na Xinhua kuhusu maafa hayo, mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga amesema mbali na vifo, idadi ya watu waliojeruhiwa ni 85, na kwamba shughuli za uokoaji zinaendelea, ambapo kikosi maalum cha uokoaji kutoka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania kiliungana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama katika harakati za kuwatafuta na kuwaokoa watu Jumapili jioni.

Akitaja maafa hayo kama "ya kuogopesha," Sendiga alisema kuwa kijiji kimoja kimemezwa kabisa na matope, na kueleza kuwa kuna uwezekano wa kuongezeka kwa idadi ya vifo na majeruhi.