Kundi la Hamas lasema watu 700 wameuawa na jeshi la Israel katika Ukanda wa Gaza ndani ya saa 24 zilizopita
2023-12-04 10:19:05| CRI

Mfanyakazi wa ofisi ya habari ya Kundi la Hamas la Palestina alisema watu wasiopungua 700 wa Palestina wameuawa kutokana na shambulizi la jeshi la Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza ndani ya saa 24 zilizopita.

Amebainisha kuwa kwa sasa bado kuna mamia ya watu walionasa kwenye vifusi wakisubiri kuokolewa, na watu wengi zaidi wamelazimika kukimbia makazi yao.

Habari zinasema jeshi la Israel tarehe 3 alfajiri lilifanya shambulizi la anga dhidi ya kambi mbili za wakimbizi zilizoko katikati ya Ukanda wa Gaza, na kusababisha vifo vya watu wasiopungua 32.