Watu 136 wafariki kwa mafuriko nchini Kenya
2023-12-04 11:05:36| cri

Idadi ya watu waliofariki kutokana na mafuriko nchini Kenya imeongezeka na kufikia 136.

Kwa mujibu wa Kituo cha Kukabiliana na Dharura na Maafa ya El Nino nchini humo, watu 462,160 wameathirika na mafuriko hayo mpaka kufikia Ijumaa iliyopita.

Katibu Mkuu wa Usalama wa Ndani wa Kenya Raymond Omollo amesema tani 10 za chakula zimesafirishwa kwa ndege hadi Kaunti ya Wajir, ambayo ni moja ya Kaunti zilizoathirika zaidi na mafuriko hayo.