Jeshi la Kanda ya EAC laanza kuondoka DR Congo
2023-12-04 10:27:06| CRI

Jeshi la Kanda ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) limeanza kuondoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Jumapili.

Kikosi cha Kenya, ambacho ni sehemu ya Kikosi cha Kanda ya EAC, kiliondoka kwenye uwanja wa ndege wa Goma Jumapili asubuhi, kufuatia uamuzi wa mamlaka ya DRC kuona kuwa jeshi la kikanda halifanyi kazi.

Baada ya mkutano wa kilele uliofanyika Novemba 25, EAC ilitangaza rasmi kwamba DRC haitaongeza muda wa mamlaka ya jeshi la kikanda zaidi ya Disemba 8, 2023.

Tangu Novemba 2022, jeshi hili la kikanda, linalojumuisha askari kutoka Uganda, Burundi na Sudan Kusini, limewekwa katika eneo la mashariki mwa DRC ili kukabiliana na migogoro iliyoibuka kati ya jeshi la DRC na waasi wa M23.

Rais wa Kongo Felix Tshisekedi anakusudia kubadilisha Jeshi la Kanda ya EAC na kikosi kilichotumwa na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC). Hata hivyo, maelezo kuhusu upelekaji wa kikosi hicho bado hayako wazi, huku mipango inayoonesha kupelekwa ndani ya miezi michache ikiwa haina ufafanuzi maalum.