Libya na UNICEF zasaini mpango kazi wa kuimarisha mifumo ya ulinzi wa watoto
2023-12-04 23:04:13| cri

Serikali ya Libya na Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) zimesaini waraka wa mpango kazi wa kuimarisha mifumo ya ulinzi na haki za watoto nchini Libya.

Taarifa iliyotolewa na UNICEF imesema, makubaliano hayo yaliyofikiwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Libya, yanalenga kufanyia mageuzi mfumo wa haki za watoto nchini humo kuendana na Makubaliano ya Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Mtoto.

Taarifa hiyo imesema, mpango kazi huo utasaidia kuboresha huduma za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Libya katika ulinzi wa watoto kupitia msaada wa kiufundi, mafunzo, na kuanzishwa kwa taasisi na mchakato utakaokuwa na msingi sahihi kuhusu haki za watoto.