Idadi ya wagonjwa wa kipindupindu nchini Sudan yaongezeka kwa asilimia 70 huku vifo vikifikia 160
2023-12-05 10:30:11| CRI

Wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa Jumatatu waliripoti kuongezeka kwa wagonjwa wa kipindupindu kwa asilimia 70 nchini Sudan ambayo inakumbwa na mapigano, na kusababisha kuongezeka kwa mwitikio.

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) imeonya kuwa mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu unaendelea kuwa mbaya zaidi, huku ongezeko jipya likiwa kubwa zaidi katika wiki tatu zilizopita.

Ikinukuu takwimu kutoka Wizara ya Afya ya Sudan na Shirika la Afya Duniani (WHO), OCHA ilisema hadi kufikia Jumatatu, karibu watu 5,200 wameshukiwa kuwa na kipindupindu, ikiwa ni pamoja na zaidi ya watu 160 waliofariki, wameripotiwa katika majimbo tisa nchini Sudan tangu Septemba 26.

OCHA imesisitiza kuwa Umoja wa Mataifa na washirika wa misaada ya kibinadamu wanaendelea zaidi kushughulikia mlipuko huo, ikiwa ni pamoja na kusaidia utambuzi na matibabu ya watu na kushughulikia masuala ya maji na usafi.