Rais Xi Jinping wa China akutana na mwenzake wa Belarus
2023-12-05 10:24:22| CRI

Rais Xi Jinping wa China jana tarehe 4 Desemba amekutana na rais Alexander Grigoryevich Lukashenko wa Belarus.

Rais Xi amesema, China na Belarus zilifikia maafikiano muhimu ya kuhimiza uhusiano kati ya nchi hizo mbili kuendelezwa kwa kiwango cha juu wakati rais Lukashenko wa Belarus alipofanya ziara nchini China mwishoni mwa Februari. Rais Xi amesema China inakaribisha Belarus kuendelea kushiriki kwenye ujenzi wa Ukanda Mmoja Njia Moja, na kupata fursa nyingi zaidi halisi za maendeleo.

Kwa upande wake Rais Lukashenko amesema, nchi yake ina imani kubwa na China kuendelea kujiendeleza, hii itasaidia mambo ya amani na maendeleo ya dunia nzima. Ameongeza kuwa, Belarus inashikilia kuendeleza uhusiano wa kirafiki kati yake na China, inapenda kuongeza mawasiliano ya ngazi ya juu kati ya pande mbili, kuendelea kuungana mkono, kupanua ushirikiano wa kunufaishana, kuimarisha uratibu wa kimkakati wa kimataifa na wa pande nyingi, na kuhimiza uhusiano wa kimkakati na kiwenzi wa pande zote kati ya Belarus na China kupata maendeleo makubwa zaidi.

Pia amesema Belarus inaamini kuwa mapendekezo yaliyotolewa na rais Xi Jinping likiwemo pendekezo la kujenga kwa pamoja Ukanda Mmoja Njia Moja ni mambo halisi ya kukusanya maoni ya pamoja ya jumuiya ya kimataifa na ushirikiano, Belarus itaendelea kujiunga kwa juhudi zote.