China yafanikiwa kurusha satelaiti ya Egypt-2
2023-12-05 10:17:37| CRI

China imerusha kwa mafanikio setilaiti ya Egypt-2 angani kwa kutumia roketi ya kubeba Long March 2C katika Kituo cha Urushaji wa Satellite cha Jiuquan . Misheni hii pia imebeba na kurusha kikundi cha pili cha satelaiti za Xingchi-1 A na B.

Satelaiti ya Egypt-2 inatumika zaidi katika sensa ya rasilimali za ardhini za Misri ili kukidhi mahitaji ya Misri katika nyanja za kilimo, misitu, ujenzi wa miji, mazingira na ufuatiliaji wa maafa. Satelaiti nyingine mbili zitatumika katika kutoa huduma za kutambua kwa mbali kwa watumiaji.