Msomi wa China: kuaga dunia kwa Henry Kissinger kutachochea mahusiano ya kimataifa kufungua zama mpya
2023-12-05 14:58:23| cri

Msomi mashuhuri wa China Prof. Huang Renwei amesema, Bw. Henry Kissinger anawakilisha zama moja, lakini kuaga dunia kwake hakumaanishi mwisho wa zama hiyo, badala yake kutachochea mahusiano ya kimataifa kufungua zama mpya.

Naibu mkurugenzi wa kudumu wa Taasisi ya Utafiti ya “Ukanda Mmoja, Njia Moja” na Usimamizi wa Dunia katika Chuo Kikuu cha Fudan Prof. Huang Renwei amesema, Bw. Kissinger siku zote alikuwa anazingatia utulivu wa kimkakati wa dunia, na kutarajia kuwepo kwa uongozi wa dunia wenye maono ya mbali. Amesema, Bw. Kissinger alikuwa ni rafiki mkubwa wa China, ambaye alitembelea China zaidi ya mara mia moja. Prof. Huang akimnukuu Bw. Kissinger amesema, bila kujali kuna matatizo mengi kiasi gani, kwa kufungua mlango na kufanya mazungumzo, hakika tutaweza kupata njia ya kutatua changamoto.