Watu wanne wafariki kwa kipindupindu nchini Tanzania
2023-12-05 10:42:37| cri

Watu wanne wamefariki kutokana na ugonjwa wa kipindupindu katika kijiji cha Buchurago kata ya Bugorora wilayani Missenyi mkoani Kagera nchini Tanzania, huku wengine wanne wakilazwa katika Hosptali ya St.Tereza.

Mkuu wa Mkoa Kagera, Fatma Mwassa amesema serikali inaendelea na uchunguzi kwa watu wote waliowasiliana kwa karibu na wagonjwa ili kuona kama wana dalili za kupata ugonjwa huo, na tayari sampuli 18 zimechukuliwa tangu ugonjwa huo ulipotokea Novemba 29 mwaka huu.

Bi. Mwassa ametoa wito kwa wananchi kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huo.