Serikali ya Tanzania yapiga hatua kudhibiti vifo vya mama wajawazito
2023-12-05 11:01:44| cri

Serikali ya Tanzania imefanikiwa kupunguza idadi ya vifo vya mama wajawazito kutoka 556 mwaka 2016 hadi kufikia 104 mwaka 2022.

Hayo yamesemwa na Rais Mstaafu wa nchi hiyo, Dk. Jakaya Kikwete wakati akifungua kongamano la pili la Sayansi la Afya ya Mama na Mtoto lililofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Dk. Kikwete ameipongeza serikali ya Tanzania kwa kuweka mazingira bora ya utoaji wa huduma za afya kwa mama mjamzito na watoto wachanga, jambo ambalo limechangia kupungua kwa idadi ya vifo hivyo.

Naye Waziri wa Afya wa Tanzania, Ummy Mwalimu amesema, serikali imeweza kuboresha miundombinu ya hospitali mbalimbali pamoja na kuzipandisha hadhi baadhi ya hospitali ili kuhakikisha zinatoa huduma bora za afya.