Wiki ya maonyesho ya mavazi Afrika yaanza nchini Kenya
2023-12-05 23:40:34| cri

Maonyesho ya Pili ya Mavazi barani Afrika yameanza jana jijini Nairobi, Kenya, huku wabunifu wa mavazi kutoka nchi mbalimbali barani humo wakionyesha ubunifu wa mavazi ya asili kutoka nchi zao.

Maonyesho hayo yatakayofanyika mpaka jumamosi wiki hii, yanajumuisha mitindo ya mavazi, utamaduni na ubunifu, na yanalenga kutambulisha utajiri mkubwa wa mavazi kutoka nchi za bara hilo.

Ofisa mkuu mwandamizi wa Wiki ya Maonyesho ya Mavazi ya Afrika, Saitoti Metamei amesema, zaidi ya wabunifu 30 wa mavazi wanaonyesha mavazi yao katika tukio hilo, huku zaidi ya wanamitindo 60 wakionyesha mavazi hayo, na kuongeza kuwa wanafunzi kutoka Chuo cha Ufundi cha Delight cha jijini Nairobi ambako maonyesho hayo yanafanyika, watapata fursa ya kuonyesha mavazi waliyobuni.