China yampongeza Rajoelina kwa kuchaguliwa tena kuwa rais wa Madagascar
2023-12-05 10:20:16| CRI

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw. Wang Wenbin amesema China inampongeza Rajoelina kwa kuchaguliwa tena kuwa rais wa Madagascar.

Kwa mujibu wa matokeo ya mwisho ya uchaguzi wa rais yaliyotolewa hivi karibuni na mahakama kuu ya katiba ya Madagascar, Andry Nirina Rajoelina amechaguliwa tena kuwa rais wa Madagascar kwa kupata asilimia 58.96 ya kura.

Akizungumza na wanahabari, Wang amesema China inaamini kuwa chini ya uongozi wa rais Rajoelina, ujenzi wa nchi na maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya Madagascar hakika utapata mafanikio zaidi. Pia amesisitiza kuwa China inatilia maanani siku zote uhusiano wa kirafiki wa jadi kati ya China na Madagascar, na kwamba inapenda kushirikiana na serikali mpya ya Madagascar katika kuimarisha na kupanua mawasiliano na ushirikiano chini ya pendekezo la kujenga kwa pamoja “Ukanda Mmoja, Njia Moja” na mfumo wa FOCAC, na kuhimiza uhusiano wa kiwenzi na ushirikiano wa pande zote kati ya China na Madagascar upate maendeleo makubwa zaidi.