Idadi ya vifo kutokana na mlipuko wa volkano yaongezeka hadi 22 nchini Indonesia
2023-12-06 09:53:18| CRI

Ofisa wa idara ya uokoaji ya Indonesia tarehe 5 amesema mlipuko wa volkano ya Marapi mkoani Sumatra Magharibi umesababisha vifo vya watu 22.

Mkurugenzi wa idara ya uokoaji ya Padang, mji mkuu wa mkoa wa Sumatra Magharibi, alisema licha ya wahanga 11 waliotambuliwa hapo awali, miili mingine 11 imetambuliwa tarehe 4 na 5 kwenye sehemu tofauti. Kwa sasa bado kuna mtu mmoja asiyejulikana alipo. Polisi wa huko walisema mtu huyu alikuwepo karibu na volkano wakati ilipolipuka, hivyo kuna uwezekano kwamba amefariki.

Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa kuna watu 75 walikuwa wanapanda volkano hiyo wakati ilipolipuka tarehe 3, ambapo watu 52 wameokolewa, 12 kati yao wanapatiwa matibabu hospitalini.