Idadi ya watu waliofariki kutokana na mafuriko nchini Kenya yafikia 154
2023-12-06 11:00:10| cri

Idadi ya watu waliofariki kutokana na mvua kubwa na mafuriko ya ghafla nchini Kenya imefikia 154.

Msemaji wa serikali ya Kenya, Isaac Mwaura amesema, mafuriko hayo yaliyosababishwa na mvua za El Nino zilizonyesha sehemu mbalimbali za nchi hiyo zimesababisha barabara kushindwa kupitika, na kwamba kazi ya kusafisha barabara katika maeneo yaliyoathirika inaendelea.

Amesema mafuriko yamesababisha mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu na magonjwa mengine yanayotokana na uchafu wa maji, huku mamlaka za Afrika zikithibitisha kuwepo kwa kesi 103 za kipindupindu na vifo vya watu wawili kutokana na ugonjwa huo katika Kaunti ya Lamu.

Ameongeza kuwa, Wizara ya Kilimo nchini humo inapanga kutoa dozi 450,000 za chanjo ya ugonjwa wa ulimi wa bluu na dozi milioni 1. 4 za homa ya Bonde la Ufa kwa mifugo ili kuongeza kinga katika maeneo yaliyoathirika.