Waziri wa mambo ya nje wa China azungumza kwa simu na waziri wa mambo ya nje wa Uingereza
2023-12-06 10:57:47| cri

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi amezungumza kwa simu na mwenzake wa Uingereza David Cameron.

Katika mazungumzo hayo, Bw. Wang Yi amesema China na Uingereza zikiwa nchi wajumbe wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, zina majukumu muhimu ya kudumisha amani na utulivu duniani. Amesema maendeleo mazuri ya uhusiano kati ya China na Uingereza si kama tu yanaendana na maslahi ya kimsingi na ya muda mrefu ya watu wa nchi hizo mbili, pia yana umuhimu wa kimkakati kwa amani na ustawi wa dunia. Ameongeza kuwa, anatarajia Uingereza itapata uelewa sahihi kwa China na kushikilia vizuri mwelekeo mzuri wa maendeleo ya uhusiano kati ya pande hizo mbili.

Bw. David Cameron amesema hakuna nchi inayoweza kukabiliana na changamoto duniani peke yake, na kuongeza kuwa Uingereza inathamini juhudi za China katika kuunga mkono utaratibu wa pande nyingi, na kutarajia China kuonesha umuhimu mkubwa katika masuala ya kikanda na ya kimataifa.