Mkutano wa VVU na UKIMWI waanza nchini Zimbabwe
2023-12-06 22:59:16| cri

Mkutano wa 22 wa Kimataifa kuhusu UKIMWI na Magonjwa ya Kuambukiza ya Zinaa (STIs) barani Afrika (ICASA) umeanza jumatatu wiki hii mjini Harare, Zimbabwe.

Mkutano huo wa kikanda utakaomalizika Jumamosi wiki hii, ni jukwaa muhimu la kubadilishana uzoefu na mafunzo ya kukabiliana na UKIMWI na magonjwa mengine ya mlipuko yanayoliathiri bara hilo.

Katika hotuba yake, rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa amesema mkutao huo unawezesha bara la Afrika kutathmini majibu yake katika kupambana na Virusi Vinavyosababisha UKIMWI na UKIMWI. Amesema kuna haja ya uratibu wa ndani wa Afrika katika kukabiliana na janga hilo, na kuongeza kuwa, kuna haja ya kuandaa hatua za ndani ya Afrika za kukabiliana na magonjwa ili kuondoa mzigo wa ugonjwa huo katika bara hilo.