Nchi za Afrika zenye kipato cha kati zahimizwa kuwekeza katika rasilimali watu
2023-12-06 09:49:03| CRI

Nchi za Afrika zenye kipato cha kati zimehimizwa kuzalisha mtaji unaohitajika ili kuhimiza ukuaji wa kijamii na kiuchumi unaotokana na uvumbuzi.

Wito huo umetolewa na watunga sera, watendaji wa maendeleo na wataalam waliohudhuria semina ya mtandaoni kuhusu "Kushughulikia Mapengo na Changamoto katika Nchi za Kipato cha Kati barani Afrika" iliyoandaliwa na Tume ya Uchumi ya Umoja wa Mataifa barani Afrika (UNECA).

Katika taarifa iliyotolewa Jumatatu, UNECA ilisema, semina hiyo ilisisitiza masuala ya kuimarisha mtaji wa watu na deni la umma kama changamoto mbili kubwa ambazo nchi za kipato cha kati za Afrika zinakabiliwa nayo kwa sasa.

Kwa mujibu wa UNECA, kukosekana kwa mtaji wa binadamu ni kipengele kikuu cha mtego wa kipato cha kati, ambacho kinazilazimisha nchi kuhamia kwenye ukuaji unaotokana na uvumbuzi, ambao unahitaji mtaji wa kutosha wa binadamu.