Taasisi ya Confucius katika Chuo Kikuu cha Addis Ababa nchini Ethiopia yaadhimisha miaka 10 ya kuanzishwa
2023-12-06 09:57:55| CRI

Taasisi ya Confucius katika Chuo Kikuu cha Addis Ababa nchini Ethiopia imefanya maadhimisho ya miaka 10 tarehe 4 Chuoni hapo.

Wanafunzi kutoka Taasisi ya Confucius katika Chuo Kikuu cha Addis Ababa walicheza kung fu ya Kichina, mchezo wa vibao vya mianzi, opera ya China na ngoma ya jadi ya Ethiopia. Pia vimetolewa vitabu vya kufundishia Kichina "Habari, Wachina" papo hapo. Vitabu hivi vinafundisha kichina kwa lugha za Kiamhari na Kioromo.

Waziri wa Elimu wa Ethiopia Kola amesema katika sherehe hizo kwamba kuendeleza mawasiliano na utamaduni kati ya watu wa Ethiopia na wa China ni msingi wa ushirikiano wa kina kati ya nchi hizo mbili. Taasisi hiyo imetoa mchango chanya katika kukuza urafiki kati ya Ethiopia na China kupitia elimu ya lugha na mawasiliano ya kitamaduni.

Naye Balozi wa China nchini Ethiopia Bw. Zhao Zhiyuan amesema katika hotuba yake kwamba Taasisi ya Confucius imeendelea na kuwa jukwaa muhimu la elimu ya lugha ya Kichina nchini Ethiopia na ushirikiano wa kitamaduni na mawasiliano kati ya China na Ethiopia.