Nigeria yathibitisha raia 85 kuuawa katika mashambulizi ya kijeshi
2023-12-06 09:55:11| CRI

Jeshi la Nigeria limefanya mashambulizi ya anga Jumapili huko katika jimbo la Kaduna kaskazini mwa nchi hiyo, lakini lilishambulia makazi ya watu kwa makosa, na kusababisha vifo vya raia 85 na wengine 66 kujeruhiwa.

Msemaji wa Shirika la Usimamizi wa Dharura la nchi hiyo NEMA Halima Suleiman alipohojiwa na televisheni za huko alisema, shirika hilo limepata taarifa kamili kwamba miili ya watu 85 imefunikwa huku kazi ya uokoaji ikiendelea.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na serikali ya jimbo la Kaduna, jeshi la Nigeria limekiri makosa hayo kwenye mkutano na maofisa wa serikali.

Mashambulizi hayo ni sehemu ya operesheni za kijeshi za kuondoa magaidi katika eneo hilo. Lakini mashambulizi ya droni yalipiga makazi ya watu badala ya maeneo lengwa, na kusababisha vifo vya watu wengi.