Raia 50 wauawa katika mashambulio nchini Ethiopia
2023-12-07 23:18:53| cri

Zaidi ya raia 50 wameuawa katika mashambulio nchini Ethiopia mwezi uliopita, ikiwa ni wiki mbili baada ya kumalizika kwa mazungumzo kati ya serikali ya nchi hiyo na kundi la waasi la Oromia.

Tume ya Haki za Binadamu ya Ethiopia imesema, wapiganaji wa Jeshi la Ukombozi wa Oromo (OLA) wamewaua watu 17 na kuchoma moto vijiji katika eneo la Benishangul-Gumuz, lililo mpakani na mkoa wa Oromia.

Kundi hilo limekuwa likipambana na serikali ya Ethiopia tangu mwaka 2018 baada ya kujitenga na kundi la Harakati za Ukombozi wa Oromo (OLF) lililotangaza kuacha mapambano ya kutumia silaha.