Rais wa China ampongeza Andry Nirina Rajoelina kuchaguliwa tena kuwa rais wa Madagascar
2023-12-07 09:31:41| CRI

Rais Xi Jinping wa China ametuma salamu za pongezi kwa Andry Nirina Rajoelina kwa kuchaguliwa tena kuwa rais wa Madagascar.

Rais Xi amesema, katika miaka ya karibuni, uhusiano kati ya nchi hizo mbili unaendelea kwa kasi, matokeo mengi ya mawasiliano na ushirikiano yamepatikana kwenye sekta mbalimbali. Amesema pande hizo mbili zinaungana mkono kithabiti juu ya maslahi makuu na masuala makubwa yanayofuatiliwa nazo.

Pia rais Xi amesema, anatilia maanani sana maendeleo ya uhusiano kati ya China na Madagascar, na kupenda kushirikiana na rais Rajoelina katika kuhimiza uhusiano wa kiwenzi na ushirikiano wa pande zote kati ya nchi hizo upate maendeleo makubwa zaidi, na kuwanufaisha zaidi watu wa nchi mbili.