Botswana mwenyeji wa mkutano wa UNESCO wa ulinzi wa urithi wa utamaduni usishikika
2023-12-07 14:18:22| cri

Botswana imekuwa nchi mwenyeji wa mkutano wa 18 wa Kamati ya Maingiliano ya Kiserikali za Ulinzi wa Urithi wa Kitamaduni Usioshikika (ICH) ya Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) unaofanyika Kasane, eneo la Chobe nchini humo.

Akizungumza katika mkutano huo, rais wa Botswana Mokgweetsi Masisi amesema, kuwa mwenyeji wa mkutano huo kunaonyesha umuhimu wa Kamati hiyo katika kulinda na kutangaza urithi hai unaothaminiwa sana na nchi hiyo.

Mkutano huo ulioanza jumatatu wiki hii na unatarajiwa kumalizika jumamosi, utawezesha Kamati hiyo kutathmini mapendekezo ya tamaduni 55 zilizowasilishwa na nchi 72.